IJUE SAIKOLOJIA; ZIFAHAMU TABIA ZA MTOTO KULINGANA NA UMRI
6:05 AM
By
Ujamaa Orphanage Foundation
0
comments
Mazingira, malezi na familia ni mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa mwili na akili ya mtoto, pamoja na uwezo wake wakutatua matatizo anayokumbana nayo katika maisha yake ya kila siku.
Uwezo
wa kupambanua mambo baina ya mtoto na mtu mzima ni tofauti kabisa,
Mfano; Mama anapovaa vizuri na kutaka kuondoka, mtoto huanza kulia
akiamini kuwa mama anamuacha na hatorudi tena. Pia mtoto akiwa anachezea
mpira na ukapotea ghafla, mtoto huusahau mpira ule kabisa na kuanza
kuchezea vitu vingine. Katika hatua hii ya ukuaji, mtoto huamini kuwa
vitu vinapoondoka mbele ya upeo wa macho yake havirudi tena na endapo
vikirudi, basi mtoto hushituka sana.
Pia
mtoto anapofikia umri wa kwenda shule, tunaweza kufikiri kuwa akili
yake imekwisha kukua na anauweza wa kupambanua mambo kwa usahihi lakini,
La Hashaah!!
Mfano;
Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba, anaweza fikiri kuwa maziwa lita
moja yakiwekwa kwenye vyombo vyenye maumbo na ujazo tofauti, basi maziwa
hayo yanabadilika ujazo.
Hali
hii huendelea hadi pale mtoto anapoweza kulinganisha au kuhusianisha
taarifa alizonazo kwenye ubongo wake na zile ambazo anakutana nazo
katika maisha ya kila siku.
Sasa tuangalie TABIA MBALIMBALI WANAZOONYESHA WATOTO BAADA YA KUZALIWA;
1.Miezi 0-1; Katika
umri huu mtoto huweza kufanya tuu yale matendo yasiyo ya hiari ambayo
hajafundishwa, mfano; Kunyonya maziwa ya mamye, kufumbua macho, kufumba
macho. Pia katika umri huu, lugha kuu anayotumia mtoto ni lugha kama
kulia wakati anasikia njaa, au kutabasamu au kucheka anapofurahi.
2.Miezi 1-4; Mtoto hupenda kurudia rudia kufanya vitu ambavyo anaona vinamfurahisha,
Mfano;
Mtoto anaweza kunyonya kidole kwa mara ya kwanza bila kukusudia, lakini
baada ya muda anarudia kunyonya vidole kwa sababu aligundua anapata
raha anaponyonya vidole vyake.
3.Miezi
4-8; Mtoto huwa na tabia ya kurudia kurudia jambo kwa kusudi lakutaka
kuona matokea yakufanya kitendo hicho yatakuwa nini?
Mfano:
Mtoto hujaribu kuinua kifani(toy) cha kuchezea na kujaribu kuweka
mdomoni kusudi aone kama kinaweza kumpa raha kama anaponyonya ziwa la
mama au kidole chake.
4.
Miezi 8-12: Kwa kipindi hiki mtoto hufanya utafiti katika mazingira
yanayomzunguka. Pia wakati huu mtoto huiga vitendo au tabia anazoona kwa
watu wengine au watoto wenzake pindi anapocheza. Huweza kugundua vitu
mbalimbali na tabia zake.
Mfano;
Mtoto anaweza kugundua kuwa akiangusha kijiko kinatoa mlio kinapofika
kwenye sakafu, hivyo atajaribu kuangusha vitu vingine zaidi kama vikombe
n.k ili kujua kuwa navyo vitatoa sauti au laah. (source-
www.africabongo.com)
www.africabongo.com)
0 comments: